Amemuibia nduguye pesa na hivi sasa anataka kumrudishia nazo

Swali: Ambaye amemuibia ndugu yake baadhi ya mali na baadaye Allaah akamtunuku kutubia. Lakini hata anaogopa kurudisha pesa hizi kwa kuchelea kusitokee matatizo. Afanye nini?

Jibu: Hakuna matatizo yatayotokea Allaah akitaka. Amtafute mtu mwaminifu na amweleze ukweli wa mambo na amwambie awape familia yake. Kwa sharti mtu huyu awe ni mwaminifu wa pesa. Ikiwa jambo hili haliwezekani kuna njia nyingine: azitume kwa posta iliyodhibitiwa na aandike kwenye karatasi kwa hati isiyokuwa yake yafuatayo:

“Hizi ni pesa ambazo uliibiwa na mwizi.”

Zitakuwa zimerudi kwake.

Check Also

Pato la haramu kwa shangazi mgonjwa na muhitajiaji

Swali: Nilipata mali kwa njia ya haramu. Je, inajuzu kumpa nazo shangazi yangu ambaye ni …