Amemuahidi mke kwamba hatooa mwanamke mwingine juu yake


Swali: Kuna mwanamme amemuahidi mke wake kwamba hatooa mwanamke mwingine juu yake. Baada ya kipindi fulani akahitajia kuoa. Je, anazingatiwa kuwa amevunja ahadi akioa?

Jibu: Anatakiwa kutoa kafara juu ya kiapo chake. Hichi ni kiapo. Ameapa kuwa hatooa juu yake, jambo ambalo alilifanya. Anatakiwa kutoa kafara juu ya kiapo chake. Kuoa ni jambo linalotakikana. Haitakiwi kwake kuendelea kuacha kuoa. Anatakiwa kutoa kafara juu ya kiapo chake na atoe kafara juu ya kiapo chake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (77) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D9%81%D8%AA%D8%AD%20%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AC%D9%8A%D8%AF-25-06-1439.lite__0.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2021