Swali 9134: Kuna mtu ambaye Allaah amemruzuku mtoto wa kiume, lakini hakukaa isipokuwa siku kumi na moja tu, kisha ukafika muda wake wa kufa kabla ya baba yake kumtahiri. Baada ya hapo baba alimfanyia tohara mwanawe akiwa amekufa, kwa sababu ya juhudi yake kubwa ya kutotumbukia katika dhambi. Alifanya hivyo kwa kutokujua. Ni ipi hukumu ya jambo hilo? Je, anawajibika kutoa kafara?

Jibu: Ikiwa jambo ni kama lilivyoelezwa, basi hakuna dhambi juu yake kwa sababu alikuwa hajui. Haimpasi kufanya hivyo tena baada ya kifo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/121)
  • Imechapishwa: 21/10/2026