Amekuwa mwanafunzi wakati yuko na zaidi ya miaka 40

Swali: Kuna walioanza kutafuta elimu ukubwani na wakawa wanachuoni. Baadhi yao ni kama Ibn Hazm na al-´Izz bin ´Abdis-Salaam ambao walikuwa zaidi ya miaka arubaini. Unanasihi nini juu ya hilo na mtu mkubwa anaweza kufikia anayofikia aliye mdogo?

Jibu: Mwenye kuwa na nia nzuri na akatafuta elimu kikwelikweli na kwa uchangamfu Allaah Humtunukia hata kama atakuwa mkuwa. Hata hivyo hili ni jambo hutokea kwa nadra kwa mtu mkubwa kuwa kama mdogo. Elimu inajidhatiti vizuri katika udogo. Sisemi kuwa mtu mkubwa hawezi kujifunza; anaweza kujifunza na akawa mwanachuoni, hata hivyo hili ni nadra kutokea. Ni miongoni mwa mambo nadra kutokea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331116.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015