Amekuta mume ana maradhi ya sukari

Swali: Iwapo mmoja wa wanandoa atakuta kuwa mwenzi mwingine ana shinikizo la damu au maradhi ya kisukari, je, mwenzi huyo anaruhusiwa kufuta ndoa?

Jibu: Ikiwa hilo linamdhuru au linapunguza haki yake, basi ana haki ya kuifuta ndoa. Lakini ikiwa jambo hilo halipunguzi chochote katika haki yake, haifai kwake kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
  • Imechapishwa: 21/07/2023