Amekusanya swalah mbili kisha akafika katika mji wakati wa swalah ya pili

Swali: Kundi la watu walisafiri kutoka Riyaadh kwenda Dhahran, wakaswali Magharib na ´Ishaa wakiwa Dhahran kwa kukusanya kwa kutanguliza katika wakati wa Magharib. Kisha wakapanda ndege kuelekea Moroko. Ndege ikatua katika nchi ya Moroko na wakakuta jua bado halijazama. Je, wanapaswa kuswali tena Magharib na ´Ishaa?

Jibu: Ndio dhahiri, kwa sababu wamefika katika mji ambao wakati wa swalah bado upo. Kwa hiyo wanalazimika kuswali. Jua liliwazamia wakiwa katika mji mwingine. Hivyo wanaswali Magharib na ´Ishaa kana kwamba ni katika siku mbili tofauti.

Swali: Je, haisemekani kwamba swalah ya mwanzo inatosha?

Jibu: Hapana, haitoshi. Hii ni wajibu mpya iliyotokea kutokana na kuhama mahali.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31580/حكم-من-جمع-صلاتين-ثم-وصل-لبلد-في-وقت-الثانية
  • Imechapishwa: 07/11/2025