Amekumbuka ndani ya swalah ya ´Aswr kuwa hajaswali Dhuhr

Swali: Ikiwa mtu atakumbuka wakati wa swalah ya ´Aswr kwamba hajaswali Dhuhr?

Jibu: Aivunje na aswali Dhuhr; abadilishe nia yake na aifanye kuwa ni ya Dhuhr.

Swali: Aanze upya?

Jibu: Ndio, aanze upya.

Swali: Baada ya kuvunja, abadilishe nia?

Jibu: Aanze upya na aweke nia ya swalah ya sasa kuwa ni Dhuhr, kisha aswali ´Aswr.

Swali: Aivunje vipi?

Jibu: Kwa nia; kwa nia akiwa mahali pake, katika kusimama kwake, aivunje kwa nia na alete Takbiyr kwa nia ya Dhuhr, kisha aendelee pamoja na imamu. Baada ya hapo alipe alichokosa, kisha aswali ´Aswr baada ya hapo.

ar-Raajihiy: Aivunje kisha alete Takbiyr?

Ibn Baaz: Alete Takbiyr mpya kwa nia ya swalah iliyopita na aikamilishe, kisha aswali ile iliyompita.

Swali: Nia na Takbiyr mpya?

Jibu: Ndio, nia na Takbiyr mpya, kwa sababu amevunja ya kwanza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31575/حكم-من-ذكر-في-الفريضة-انه-ما-صلى-التي-قبلها
  • Imechapishwa: 09/11/2025