Amekumbuka baada ya siku kupita kwamba aliswali bila wudhuu´

Swali: Niliswali Dhuhr hali ya kuwa ni mwenye kuamini kuwa niko na wudhuu´ na siku ya pili ndio nikakumbuka kuwa sina wudhuu´. Ni ipi hukumu?

Jibu: Ambaye ameswali huku akidhani kuwa yuko na wudhuu´ kisha baada ya siku moja au zaidi akakumbuka kwamba hakuwa na wudhuu´, basi pindi tu atakapokumbuka atatakiwa kuirudi swalah yake ambayo ameiswali pasi na wudhuu´.  Haijalishi kitu ijapo ni baada ya mwezi au zaidi ya hapo. Pale atakapokumbuka kuwa ameswali Dhuhr, ´Aswr, Maghrib, ´Ishaa au Fajr bila ya wudhuu´ basi atatakiwa kuirudi hiyo peke yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayelala na kupitikiwa na swalah au akaisahau basi aiswali pale atakapokumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”

Twahara ni sharti ya swalah. Hivyo basi akiswali pasi na twahara atatakiwa kuirudi kwa maafikiano. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah haikubaliwi pasi na twahara.”

“Swalah ya mmoja wenu haikubaliwi akipatwa na hadathi mpaka atawadhe.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4557/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%B5%D9%84%D9%89-%D9%8A%D9%88%D9%85%D8%A7-%D8%A8%D9%84%D8%A7-%D9%88%D8%B6%D9%88%D8%A1-%D8%AC%D9%87%D9%84%D8%A7-%D8%A8%D8%AD%D8%AF%D8%AB%D9%87
  • Imechapishwa: 07/11/2020