Swali: Niliswali ´Aswr nikiwa katika mji wangu kisha nikasafiri. Nilipokuwa njiani nikakumbuka kwamba niliiswali bila kuwa na twahara. Je, niiswali kwa kufupisha au Rak´ah nne? Na ni ipi hukumu ikiwa litafanyika kinyume chake; kwa maana kwamba baada ya kurudi kutoka safarini nikakumbuka kwamba niliswali ´Ishaa kwa kufupisha pasi na kuwa na twahara? Je, niilipe Rak´ah nne au mbili?
Jibu: Ikiwa utakumbuka ukiwa safarini kwamba uliswali ´Aswr au swalah nyingine ukiwa mkazi bila wudhuu´, basi utailipa kwa Rak´ah nne kwa sababu ilikuwajibikia Rak´ah nne. Vivyo hivyo ikiwa utakumbuka kwamba uliswali ukiwa safarini Dhuhr, ´Aswr au ´Ishaa bila wudhuu´, kisha ukakumbuka jambo hilo baada ya kuwa mkazi, basi utailipa Rak´ah nne. Kwa sababu sababu ya kufupisha swalah imeondoka, nayo ni safari.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/221)
- Imechapishwa: 16/03/2026
Swali: Niliswali ´Aswr nikiwa katika mji wangu kisha nikasafiri. Nilipokuwa njiani nikakumbuka kwamba niliiswali bila kuwa na twahara. Je, niiswali kwa kufupisha au Rak´ah nne? Na ni ipi hukumu ikiwa litafanyika kinyume chake; kwa maana kwamba baada ya kurudi kutoka safarini nikakumbuka kwamba niliswali ´Ishaa kwa kufupisha pasi na kuwa na twahara? Je, niilipe Rak´ah nne au mbili?
Jibu: Ikiwa utakumbuka ukiwa safarini kwamba uliswali ´Aswr au swalah nyingine ukiwa mkazi bila wudhuu´, basi utailipa kwa Rak´ah nne kwa sababu ilikuwajibikia Rak´ah nne. Vivyo hivyo ikiwa utakumbuka kwamba uliswali ukiwa safarini Dhuhr, ´Aswr au ´Ishaa bila wudhuu´, kisha ukakumbuka jambo hilo baada ya kuwa mkazi, basi utailipa Rak´ah nne. Kwa sababu sababu ya kufupisha swalah imeondoka, nayo ni safari.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/221)
Imechapishwa: 16/03/2026
https://firqatunnajia.com/amekumbuka-akiwa-safarini-kuwa-aliswali-aswr-bila-twahara/