Amekula kwa kudhani kuwa kumepambazuka na amefungua kwa kudhani kuwa jua limezama

Swali: Vipi swawm ya ambaye amedhani kuwa bado ni usiku…

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba atalipa siku hiyo. Akila asubuhi akidhani kuwa bado ni usiku kisha ikabaini kuwa amekula mchana, atalipa siku hiyo. Hivo ndivo wanavoona jopo kubwa la wanazuoni. Vivyo hivyo akila kwa kudhani kuwa jua limekwishazama kisha ikabaini kinyume chake, atalazimika kulipa kwa mujibu wa kikosi kikubwa cha wanazuoni.

 Swali: Baadhi wanasema ni ipi dalili?

Jibu: Dalili ni kwamba imebainika kuwa ni mchana. Ni wajibu wake kufunga mchana mzima na sasa imedhihiri kuwa amekula mchana. Ilimpasa asizembee, ajitahidi na achukue tahadhari na asiharakishe kufungua swawm na sambamba na hilo asicheleweshe kula. Jengine ni kwamba mlango huu ukifunguliwa itakuwa ni mtihani mkubwa na watu kuchukulia wepesi.

Swali: Hali hiyo si iliwahi kumtokea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Imesemekana kwamba walilipa na imesemekana kinyume chake. Baadhi ya Salaf wamesema, kwa mujibu wa Hadiyth ya Asmaa´, ya kwamba ni lazima kulipa. Kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kuwa ni lazima kulipa na baadhi yao wamesema kuwa hakuna kulipa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24417/ما-حكم-صوم-من-اكل-ظانا-بقاء-الليل
  • Imechapishwa: 08/10/2024