Amekosa maji baada ya ada yake ya mwezi

Swali: Baada ya mwanamke kusafika kutoka katika ada yake ya mwezi, alikosa maji ya kutosha kwa ajili ya kuoga. Je, ajitwaharishe kwa udongo na kuswali? Je, inafaa baada ya hapo kwa mume wake kumjamii? Ikiwa baada ya mume wake kumjamii akapata maji, je, atalazimika kuoga kwa ajili ya hedhi na jimaa au inatosha kujitwaharisha kwa udongo na kuoga kwa ajili ya janaba?

Jibu: Akisafika na asipate maji, basi atajitwaharisha kwa udongo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

“… kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum kwa ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[1]

Baada ya hapo itafaa kwake kuswali na kuingiliwa na mume wake. Akipata maji, basi atanuia kuoga kwa ajili ya hedhi na jimaa. Kwa maana nyingine haitoshi kujitwaharisha kwa udongo kwa ajili ya hedhi. Kwa mujibu wa maoni sahihi ni kwamba kujitwaharisha kwa udongo ni jambo linalofaa na si lenye kuondosha najisi.

[1] 05:06

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 431
  • Imechapishwa: 21/07/2025