Amekatisha ´Umrah yake kwa sababu ya msongamano

Swali: Mtu alinuia kufanya ´Umrah kisha akahirimia kutoka kwenye kituo. Baada ya kuingia Haram akakuta msongamano akarudi nyumbani kwake akavaa nguo zake na hakufanya ´Umrah katika Ramadhaan iliopita. Nini kinachomlazimu pamoja na kuzingatia kwamba bado hajaoa?

Jibu: Anapaswa kukamilisha ´Umrah. Bado yuko katika Ihraam. Kwa hiyo inampasa aende atufu, aafanye Sa´y, apunguzwe nywele na kutoka kwenye Ihraam. Ikiwa alikuwa mjinga, basi hakuna juu yake kitu kwa upande wa kuvaa nguo kwa sababu ya ujinga wake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31065/ما-حكم-من-احرم-ولم-يعتمر-بسبب-الزحام
  • Imechapishwa: 27/09/2025