Amejua kuwa ameswali na najisi baada ya kumaliza swalah

Swali: Alijua najisi kwenye nguo yake mwanzoni, lakini akaswali akiwa amesahau?

Jibu: Hakuna tatizo:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

Swali: Vipi kama alijua kuhusu najisi mwanzoni lakini akaichelewesha kwa sababu fulani, kisha akasahau na kuswali?

Jibu: Ndio, swalah yake ni sahihi.

Swali: Ikiwa atajua kuhusu najisi wakati wa swalah, nayo ipo kwenye nguo zake za ndani?

Jibu: Swalah yake inabatilika; anatakiwa kuivua, kuibadilisha au kuisafisha. Swalah yake inabatilika. Lakini kama hakujua mpaka baada ya kumaliza swalah, basi swalah yake ni sahihi.

[1] 02:286

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31570/ما-حكم-من-صلى-ناسيا-نجاسة-في-ثوبه
  • Imechapishwa: 06/11/2025