Amefupisha Maghrib Rak´ah mbili

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu aliyeswali Maghrib huko Muzdalifah Rak´ah mbili?

Jibu: Anatakiwa kuirudia. Ikiwa ameswali Maghrib Rak´ah mbili, hilo halijuzu. Kwa sababu Maghrib haifupishwi kwa maafikiano ya waislamu. Kwa hiyo ni wajibu kwake kuiswali tena Rak´ah tatu kisha aiswali tena ´Ishaa pamoja nayo, kwa sababu swalah ya ´Ishaa haisihi isipokuwa baada ya Maghrib. Kwa hiyo ataswali tena Maghrib Rak´ah tatu, kisha ataswali tena ´Ishaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/198)
  • Imechapishwa: 12/03/2026