Amechangisha pesa kwa ajili ya kuoa akaenda nazo kuhiji

Swali: Unasemaje juu ya mtu ambaye amehiji kwa ajili ya Allaah (Ta´ala) ile hajj ya kwanza ya faradhi kwa kiwango fulani cha pesa ambacho alikipata pindi alipokuwa anataka kuoa na akawa si muweza. Ni fakiri. Baadhi ya wanachuoni wakamsaidia kwa kumpa kiwango fulani cha pesa. Kisha akachukua sehemu ya pesa hizo ambazo zilikuwa zimsaidie kuhiji na akahiji hajj ya faradhi na mpaka sasa bado hajahiji. Mambo haya yalipitika mwaka ulopita na mtu huyo mpaka sasa hajaoa. Ni ipi hukumu ya hajj yake?

Jibu: Kuhusu hajj yake ni sahihi. Lakini kitendo chake ni cha kimakosa. Kinachompasa hivi sasa ni lazima kwake kwenda kwa yule mtu aliyemsaidia juu ya kuoa na amfahamishe ukweli wa mambo. Amwambia kwamba alihiji kwa baadhi ya pesa alizompa. Nataraji mtu huyo ambaye alimsaidia atamsamehe. Hivyo atakuwa amepata thawabu mara mbili:

1- Thawabu za kumsaidia kuhiji.

2- Thawabu za kumsaidia kuoa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1195
  • Imechapishwa: 20/07/2019