Swali: Vipi kwa mwenye kuapa kuacha maasi fulani kisha akarejea katika maasi hayo?

Jibu: Analazimika kutubia kwa Allaah na atoe kafara ya kiapo vyote viwili. Asirejee. Haijuzu kwake kurejea. Kwa mfano akiapa kwamba hatokunywa tena pombe, hatovuta tena sigara na kwamba hatowaasi tena wazazi wawili. Mambo hayo yanamlazimu hata kama hakuapa. Lakini akiapa anazidi kutilia nguvu mambo hayo. Katika hali hiyo atalazimika kujizuia kutokamana na maasi. Akipewa mtihani huo basi atalazimika kutoa kafara ya kiapo na kutubia vyote viwili. Atalazimika kutoa kafara ya kiapo, tawbah na kujutia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24408/حكم-من-حلف-ان-يترك-معصية-ثم-رجع-لها
  • Imechapishwa: 07/10/2024