Ameacha wasia wa kuzikwa kwenye msikiti aliyojenga

Swali: Mtu anayejenga msikiti, halafu akawaamuru watu wamzike humo kwa kutumia kipimo juu ya kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hapana, hazikiwi ndani yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuzikwa ndani ya msikiti. Mtume alizikwa kwenye chumba chake, ndani ya nyumba yake. Lakini wakati al-Waliyd alipopanua msikiti, aliingiza kile chumba na kukifanya kuwa sehemu ya msikiti. Kwa hiyo Mtume hakuzikwa ndani ya msikiti, bali alizikwa ndani ya nyumba ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Lakini baadhi ya watawala wa karne ya kwanza waliingiza kile chumba chote ndani ya msikiti kwa ajili ya upanuaji, jambo ambalo lilikuwa kosa kutoka kwao. Lakini tayari maji yamekwishamwagika.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1133/بنى-مسجدا-واوصى-ان-يدفن-فيه
  • Imechapishwa: 03/01/2026