Ameacha kufunga Ramadhaan kwa kulazimika kutafuta maisha kwa ajili yake na familia yake

Swali 397: Kuna mwanaume aliacha kufunga Ramadhaan kwa sababu ya kutafuta chumo la maisha yake na chumo la wale dhuriya yake walioko chini yake. Ni ipi hukumu?

Jibu: Kama ambavo inafaa kwa mgonjwa kuacha kufunga inajuzu vilevile kwa yule asiyeweza kuishi isipokuwa kwa kuacha kufunga akala. Huyu ni Muta´wil na alipe Ramadhaan akiwa yukohai au afungiwe akiwa ameshakufa. Asipofungiwa basi anatakiwa kutolewa chakula kumpa masikini kwa kila siku moja aliyoacha kufunga.

Ama akiacha pasi na Ta´wiyl, basi maoni yenye nguvu ya wanachuoni ni kwamba kila mtu akikusudia kuichelewesha ´ibaadah iliyowekewa muda maalum pasi na udhuru, basi haikubaliwi kutoka kwake. Itamtosha kwake kufanya matendo mema, swalah nyingi za sunnah na kuomba msamaha. Dalili ya hilo ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika yale yaliyosihi kutoka kwake:

”Mwenye kufanya matendo yasiyoafikiana na amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”

Kama ambavo ´ibaadah zilizowekewa wakati wake haziwezi kufanywa kabla ya wakati wake vivyo hivyo hazifanywi baada ya wakati wake. Ama kukiwa kuna udhuru kama ujinga au kusahau, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu ya yule aliyesahau:

“Mwenye kupitiwa na usingizi swalah ikampita au akaisahau, basi aiswali atapokumbuka. Hakuna kafara yake isipokuwa hiyo.”[1]

Pamoja na kwamba kunahitajia ufafanuzi zaidi kuhusu mjinga na hapa si mahala pa kuyataja hayo.

[1] Muslim (314).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 455-456
  • Imechapishwa: 05/05/2019