Ambaye anaswali Dhuhr nyuma ya imamu anayeswali ´Aswr

Swali: Mtu ambaye ni msafiri amerejea na kuchelewesha swalah, kisha akaswali kwa nia ya ´Aswr huku bado hajaswali. Je, swalah yake ni sahihi au anapaswa kuirudia?

Jibu: Sahihi ni kwamba anapaswa kuirudia. Ataswali Dhuhr kwanza, kisha baadaye ndio aswali ´Aswr. Hata hivyo ikiwa ataswali pamoja na wengine ili kupata fadhilah za mkusanyiko, swalah hiyo itahesabika kama swala ya kujitolea na baada ya hapo ataswali Dhuhr kisha ´Aswr. Ikiwa ataswali Dhuhr pamoja nao kwa nia ya Dhuhr huku wao wanaswali ´Aswr, swalah hiyo inakubalika kwa mujibu wa maoni sahihi. Jopo la wanazuoni wamechagua maoni hayo kama vile al-Muwaffaq, Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na wengineo. Ataswali kwa nia ya Dhuhr wakati wao wanaswali ´Aswr, kisha baada ya kumaliza ataswali ´Aswr.

Swali: Katika hali hiyo nia zimetofautiana?

Jibu: Haidhuru kule kutofautiana kwa nia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24781/حكم-من-صلى-العصر-مع-جماعة-وعليه-الظهر
  • Imechapishwa: 17/12/2024