Ambaye amenuia kufunga kisha akawa mgonjwa

Swali: Kuna mtu alinuia kufunga Sha´baan na katikati ya funga yake ya Sha´baan akapatwa na maradhi ambapo akala na katika nia yake ni kukamilisha kuifunga Sha´baan. Je, analipwa kwa alichonuia?

Jibu: Kunatarajiwa atalipwa kwa alichonuia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu anapokuwa mgonjwa au akasafiri, basi Allaah anamwandikia mfano wa aliyokuwa akiyafanya katika hali ya ukazi na uzima.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika si vyenginevyo kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia.”[2]

[1] al-Bukhaariy (2996).

[2] al-Bukhaariy (01).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/421)
  • Imechapishwa: 19/04/2022