Ambaye amekosa baadhi ya Takbiyr katika swalah ya jeneza

325 – Nilimuuliza Shaykh wetu kuhusu mtu aliyekosa baadhi ya Takbiyr katika swalah ya jeneza?

Jibu: Atakamilisha Takbiyr kwa mfululizo; ili jeneza lisichukuliwe kabla hajamaliza. Ikiwa amekosa al-Faatihah, basi aisome, kisha alete Takbiyr, kisha aseme:

اللهم صل على محمد

”Ee Allaah msifu Muhammad… ”

Kisha alete Takbiyr, kisha aseme:

اللهم اغفر له

”Ee Allaah! Msamehe.”

Kisha alete Takbiyr na kadhalika. Kwa maana afanye haraka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 116
  • Imechapishwa: 29/05/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´