Swali: Mara nyingi tunasikia watu wakisema “Allaah na Mtume”. Nini maana ya maneno hayo? Je, ni shirki?

Jibu: Ni shirki ya matamshi. Ikiwa mtu huyo anakusudia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mshirika wa Allaah, ni kafiri. Na ikiwa amesema hivo pasi na kukusudia, kitendo hicho ni shirki ya matamshi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiseme. “Akitaka Allaah na akataka Muhammad”. Sema: “Akitaka Allaah pekee”.”[1]

Kwa hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asishirikishwe pamoja na Allaah (´Azza wa Jall). Kila mmoja awekwe nafasi yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anayo nafasi Yake ya juu inayolingana Naye, na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anayo nafasi yake ya juu inayolingana na utume wake.

[1] Ibn Maajah (2118), Ahmad (20713), Ibn Hibbaan (5725), al-Haakim (5945) na at-Twabaraaniy (8214). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Ibn Maajah” (1721).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 294
  • Imechapishwa: 27/04/2025