Swali: Je, nafsi ni sifa ya Allaah kama sifa Zake zingine?

Jibu: Ndio, kwa namna inavyomstahikia Yeye. Hakuna anayejua namna yake isipokuwa Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala).

Mwanafunzi: Kwa maana ya kwamba sifa ya nafsi sio dhati?

Ibn Baaz: Ndio, sio dhati:

تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ

”Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala mimi sijui yale yaliyomo katika nafsi Yako.”[1]

Mwanafunzi: Baadhi ya ndugu waliopo wameandika swali kuhusu hili?

Ibn Baaz: Nafsi ni tofauti na dhati. Dhati ni kitu na nafsi ni kitu kingine. Hakuna yeyote mwenye ghera zaidi kuliko Allaah. Hakuna yeyote (شخصَ) mwenye ghera zaidi kuliko Allaah.

Mwanafunzi: Lakini kumepokelewa andiko kuhusu dhati?

Ibn Baaz: Ndio, maandiko yote ni kuhusu dhati:

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ

”Allaah ni Muumbaji wa kila jambo.”[2]

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ

“Hakika Mola wenu ni Allaah… ”[3]

Yote haya yanarudi katika dhati. Hata hivyo ni Mwenye kusifiwa kwa dhati pia.

Mwanafunzi: Nini maana ya dhati katika lugha?

Ibn Baaz: Ni hakika ya kitu. Dhati ya kitu ni hakika yake.

[1] 05:116

[2]39:62

[3] 7:54

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31063/هل-النفس-صفة-لله-عز-وجل-كساىر-الصفات
  • Imechapishwa: 27/09/2025