Alipe siku zake wakati wa majira ya baridi

Swali: Ni kipi kinachomlazimu mwanamke anayenyonyesha aliyeacha kufunga kwa kuchelea juu ya mtoto wake?

Jibu: Hakuna kitu kinachomlazimu mwanamke anayenyonyesha akila kwa sababu ya kuchelea juu ya mtoto wake kupungua kwa maziwa. Atalipa baada ya hapo. Lakini baadhi ya wanazuoni wanasema ikiwa kuacha kwake kufunga ni kwa sababu ya kukhofia juu ya mtoto peke yake, yule mtu ambaye anawajibika kumhudumia mtoto, kama vile baba au ndugu yake, itamlazimu kulisha masikini kwa kila siku moja aliyoacha kufunga na yeye mwanamke atayalipa masiku aliyokula. Tukikadiria kuwa jambo hilo litamwendelea, basi haidhuru kwa sababu amepewa udhuru. Hata hivyo sidhani kuwa jambo hilo litaendelea. Kwa sababu wakati wa majira ya baridi michana inakuwa mifupi na wakati unakuwa wenye baridi, hivyo hayapungui maziwa yake iwapo atafunga. Kwa msemo mwingine atalipa masiku yaliyompita wakati wa majira ya baridi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/161)
  • Imechapishwa: 03/04/2026