al-Waadi´iy kuhusu kurefusha du´aa katika Tarawiyh na kunyanyua mikono katika Witr

Swali 15: Ni ipi hukumu ya kuomba du´aa katika swalah ya Tarawiyh? Ni upi usahihi wa Hadiyth kuhusu kunyanyua mikono katika Witr pamoja na kunitajia dalili?

Jibu: Kuhusu kuomba du´aa kwa kurefusha namna hiyo katika swalah ya Tarawiyh ni Bid´ah, Bid´ah na ni Bid´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfunza al-Hasan kusema:

اللهم اهدني فيمن هديت, وعافني فيمن عافيت, وتولني فيمن توليت, وبارك لي فيما أعطيت, وقني شر ما قضيت, فإنك تقضي ولا يقضى عليك, وإنه لا يذلّ من واليتَ, ولا يعزّ من عاديت, تباركت ربنا وتعاليت، لا منجا منك إلا إليك

“Ee Allaah! Niongoze pamoja na wale Uliowaongoza, uniafu pamoja na wale Uliowaafu, Uniangalie pamoja na wale Unaowaangalia, Unibariki katika kile Ulichotoa na Unilinde kutokamana na shari kwa yale Uliyohukumu. Kwani hakika Wewe ndiye mwenye kuhukumu na wala Huhukumiwi. Hakika hatwezeki yule Uliyemfanya mpenzi na wala hapati nguvu yule Uliyemfanya adui. Umebarikika na Umetukuka Mola wetu. Hakuna mahali pa kuokoka kutokamana na Wewe isipokuwa Kwako.”

Kadhalika yale yanayofanywa Makkah na al-Madiynah katika kurefusha ni jambo ambalo halikuwekwa katika Shari´ah. Uongofu bora ni wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kuhusu kunyanyua mikono ni jambo limepokelewa kupitia kwa ´Abdullaah bin Naafiy´ bin Abiy al-´Umyaa´ ambaye ni dhaifu. Imekuja katika “al-Musnad” ya Imaam Ahmad kupitia kwa Anas lakini asili yake iko kwa al-Bukhaariy na Muslim. Ndani yake hakukutajwa jambo la kunyanyua mikono. Sisi tuna mashaka juu ya kuthibiti kwake. Kwa hivyo jambo la kunyanyua mikono katika du´aa ya Witr ni jambo ambalo halikuwekwa katika Shari´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 138
  • Imechapishwa: 30/12/2019