Swali: Kuna mtu anafanya kazi ya uanasheria na anauliza kama kazi hiyo ni halali au haramu? Shari´ah inasemaje juu ya kazi hiyo kwa sababu anaweza kumtetea mwenye kudhulumiwa kwa kaisi cha uwezo wake? Unamnasihi nini?
Jibu: Ushauri wangu aache kazi hiyo. Kwa sababu wakati wa kutetea atatetea kwa mujibu wa kanuni na hatokubaliwa kutumia maneno ya Allaah Allaah na maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ
“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.”[1]
أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ
“Je, wanataka hukumu za kipindi cha kijahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.”[2]
Kwa hivyo namwambia kuwa ni lazima kwake kuacha kazi hiyo, kwa sababu maana yake ni kwamba anakubaliana na kanuni hizo za kikafiri na anakuwa ni mwenye kushirikiana nao. Ambaye amedhulumiwa atanusuriwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), Allaah atamlipizia kisasi dhidi ya mpinzani wake au atamuwekea akiba huko Aakhirah.
[1] 05:55
[2] 05:50
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 429-430
- Imechapishwa: 20/07/2025
Swali: Kuna mtu anafanya kazi ya uanasheria na anauliza kama kazi hiyo ni halali au haramu? Shari´ah inasemaje juu ya kazi hiyo kwa sababu anaweza kumtetea mwenye kudhulumiwa kwa kaisi cha uwezo wake? Unamnasihi nini?
Jibu: Ushauri wangu aache kazi hiyo. Kwa sababu wakati wa kutetea atatetea kwa mujibu wa kanuni na hatokubaliwa kutumia maneno ya Allaah Allaah na maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ
“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.”[1]
أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ
“Je, wanataka hukumu za kipindi cha kijahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.”[2]
Kwa hivyo namwambia kuwa ni lazima kwake kuacha kazi hiyo, kwa sababu maana yake ni kwamba anakubaliana na kanuni hizo za kikafiri na anakuwa ni mwenye kushirikiana nao. Ambaye amedhulumiwa atanusuriwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), Allaah atamlipizia kisasi dhidi ya mpinzani wake au atamuwekea akiba huko Aakhirah.
[1] 05:55
[2] 05:50
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 429-430
Imechapishwa: 20/07/2025
https://firqatunnajia.com/al-waadiiy-kuhusu-kazi-ya-uanasheria/