Nilipata wageni kutoka Algeria. Wakanambia kuwa al-Ghazaaliy na al-Qardhwaawiy waliwaendea kwenye chuo kikuu cha Algeria. Wasichana na wavulana walikuwa wakihisi uchungu kuchanganyika. Ndipo al-Qardhwaawiy akasema kuwa ni lazima kwa mwanamke kusoma na kwamba amemtuma msichana wake mmoja nje ya nchi, mmoja Kuwait na mwingine sehemu nyingine.
Inahusiana na kulingania katika upotevu. Inahusiana na kuwapaka mchanga wa machoni wanafunzi wa kialgeria. Himdi zote ni za Allaah walifahamu malengo yake machafu. Wakaanza kumchukia na kumkimbia.
Ni wajibu, wajibu kwa wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah kukusanya kaseti na magazeti yake ambapo mna maneno yake na wawabainishie waislamu hali yake. Ni lazima kutolewe kanda na vitabu kati ya waislamu inayomsaga kama alivyosagwa at-Twahhaan kwenye kitabu “Iqaamat-ul-Burhaan ´alaa Dhwalaal ´Abdir-Rahmaan at-Twahhaan”. Baadhi ya vijana Misri wanakinunua kitabu na wanashangazwa na kichwa cha khabari hiki. Mambo gani haya? al-Waadi´iy anasema kuwa mlinganizi mkubwa kama ´Abdur-Rahmaan at-Twahhaan ni mpotevu?!?! Himdi zote ni za Allaah mambo yametulia. Jumuiya ya kiyemeni al-Hikmah – Allaah asiibariki – inasema kuwa at-Twahhaan ni mwanachuoni na mtu muheshimiwa ambaye ana makosa kama wengine walivyo na makosa.
Midhali haki imekubainikia wewe usijali yule mwenye kwenda kinyume na wewe. Kuwa mlaini kwa wale wanachuoni waheshimiwa. Usiwaponde wale wanachuoni waheshimiwa hata kama wataona kuwa umekosea. Wakikuraddi bado unatakiwa kuwa mpole kwao. Mpe kila mmoja haki yake anayostahiki.
Kuhusiana na mtu ambaye kila siku analeta mabalaa, ni wajibu kuwabainishia waislamu hali yake ili wajihadhari naye. Ni wajibu kwa Qatar istahi na imtimue mwanaume huyo mfisadi na mwenye kufisidi [Yuusuf al-Qardhwaawiy].
- Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 11-13
- Imechapishwa: 08/10/2016
Nilipata wageni kutoka Algeria. Wakanambia kuwa al-Ghazaaliy na al-Qardhwaawiy waliwaendea kwenye chuo kikuu cha Algeria. Wasichana na wavulana walikuwa wakihisi uchungu kuchanganyika. Ndipo al-Qardhwaawiy akasema kuwa ni lazima kwa mwanamke kusoma na kwamba amemtuma msichana wake mmoja nje ya nchi, mmoja Kuwait na mwingine sehemu nyingine.
Inahusiana na kulingania katika upotevu. Inahusiana na kuwapaka mchanga wa machoni wanafunzi wa kialgeria. Himdi zote ni za Allaah walifahamu malengo yake machafu. Wakaanza kumchukia na kumkimbia.
Ni wajibu, wajibu kwa wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah kukusanya kaseti na magazeti yake ambapo mna maneno yake na wawabainishie waislamu hali yake. Ni lazima kutolewe kanda na vitabu kati ya waislamu inayomsaga kama alivyosagwa at-Twahhaan kwenye kitabu “Iqaamat-ul-Burhaan ´alaa Dhwalaal ´Abdir-Rahmaan at-Twahhaan”. Baadhi ya vijana Misri wanakinunua kitabu na wanashangazwa na kichwa cha khabari hiki. Mambo gani haya? al-Waadi´iy anasema kuwa mlinganizi mkubwa kama ´Abdur-Rahmaan at-Twahhaan ni mpotevu?!?! Himdi zote ni za Allaah mambo yametulia. Jumuiya ya kiyemeni al-Hikmah – Allaah asiibariki – inasema kuwa at-Twahhaan ni mwanachuoni na mtu muheshimiwa ambaye ana makosa kama wengine walivyo na makosa.
Midhali haki imekubainikia wewe usijali yule mwenye kwenda kinyume na wewe. Kuwa mlaini kwa wale wanachuoni waheshimiwa. Usiwaponde wale wanachuoni waheshimiwa hata kama wataona kuwa umekosea. Wakikuraddi bado unatakiwa kuwa mpole kwao. Mpe kila mmoja haki yake anayostahiki.
Kuhusiana na mtu ambaye kila siku analeta mabalaa, ni wajibu kuwabainishia waislamu hali yake ili wajihadhari naye. Ni wajibu kwa Qatar istahi na imtimue mwanaume huyo mfisadi na mwenye kufisidi [Yuusuf al-Qardhwaawiy].
Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 11-13
Imechapishwa: 08/10/2016
https://firqatunnajia.com/al-qardhwaawiy-anashajiisha-wanawake-wakasome-kwenye-vyuo-vikuu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)