al-Qaradhwaawiy hawezi kulinganishwa na mwanafunzi hata mmoja wa Ibn Baaz

Vilevile inahusiana na pindi Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah). Wakati alipotoa fatwa kuhusu mkataba wa amani na mayahudi ili waislamu waweze kuishi kwa usalama. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya mkataba na washirikina na akafikia mpaka kupakana nao mafuta katika baadhi ya mambo. Hivyo baadhi ya watu wakakasirika na kuanza kuleta matatizo na kulaani. Wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah, wanafunzi na wahubiri kamwe hawawatukani wanachuoni.

Kuna Khatwiyb mmoja Swan´aa´ alimkemea Shaykh Ibn Baaz. Allaah amrehemu Shaykh Ibn Baaz. Baada ya ijumaa karibu watu wote wakatoka nje ya msikiti na huku wanamuomba Allaah amlaani Shaykh Ibn Baaz. Wakati muhubiri huyu mfanya mapinduzi alipoulizwa juu ya hilo, akasema kuwa amemkemea kwa maneno ya al-Qaradhwaawiy! Ndipo mtu mmoja aliyekuwepo pale akasema:

“Ukatakasifu ni Wako Allaah! al-Qaradhwaawiy ni nani ukilinganisha na Shaykh Ibn Baaz?”

Shaykh Ibn Baaz ni ´Allaamah, kiongozi wa wanachuoni, Muftiy wa nchi yote, kiongozi wa wanachuoni na kiongozi wa Muftiyyuun, marejeo ya Ummah. al-Qaradhwaawiy halingani hata na mwanafunzi wake. Shaykh Ibn Baaz ana wanafunzi ambao ni vigogo. Shaykh [´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah] ar-Raajhiy ni mmoja katika mfano wa wanafunzi wa Shaykh Ibn Baaz. Hawa ni maimamu! al-Qaradhwaawiy hawezi kulinganishwa hata na mwanafunzi mmoja miongoni mwa wanafunzi wa Shaykh Ibn Baaz, lakini:

فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ

“Hakika si venginevyo hayapofuki macho, lakini zinapofuka nyoyo ziliomo vifuani.” (22:46)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/Dars-13304
  • Imechapishwa: 26/08/2020