al-Khaliyliy akitumia dalili ya shairi la mnaswara juu ya kupinga maneno ya Allaah

al-Khaliyliy ametumia dalili vilevile maneno na mashairi ya al-Akhtwal [kuthibitisha kuwa Qur-aan ni maneno yaliyosimama kwenye nafsi ya Allaah]. Hata kama tutachukulia kama kweli maneno hayo ya al-Akhtwal yamethibiti, mtu atastaajabu namna al-Khaliyliy anavyotumia hoja kwa maneno ya al-Akhtwal ambaye alikuwa mnaswara, kafiri na mpotevu katika ´Aqiydah yake na katika maneno ya Allaah [al-Khaliyliy] anayapotosha maneno ya Allaah yaliyo ya wazi kwa maneno ya mnaswara ambayo yamekuja kwa tamko “neno” hali ya kukariri katika Aayah hii ambayo yanasomwa na kusikiwa. Allaah (´Azza wa Jall) anasema katika Aayah hii tukufu:

إِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَيْءٍ إِذَا أَرَدْنَاهُ أَن نَّقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ

“Hakika Kauli Yetu juu ya kitu tunapokitaka hukiambia: “Kuwa!” – basi kinakuwa.”[1]

Kweli tamko hili [la Aayah] linaendana na taarifu ya al-Khaliyliy kuhusu kwamba [maneno ya Allaah] ni maneno yaliyo kwenye nafsi yasiyokuwa na herufi wala sauti na ambayo hayakusikiwa na yeyote na kwamba ni maneno tu yaliyosimama kwenye nafsi ya yule mzungumzaji.

Hakika miongoni mwa kukoseshwa nusura ni muislamu kutumia dalili maneno ya mnaswara ambaye amepotea katika ´Aqiydah yake na katika maneno ya Allaah (´Azza wa Jall) yanayosomwa na yanayosikizwa kama alivyosema (Ta´ala):

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ

“Ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah.”[2]

Kuhusu manaswara wao wenyewe wamepotea katika maana ya maneno na wamedai ya kwamba ´Iysaa (´alayhis-Salaam) yeye mwenyewe ndiye neno la Allaah na wakachukua kitu kutoka kwa mungu kutoka kwenye kitu katika watu. Hivi kweli mtu atatumia dalili maneno ya mnaswara, ambaye amepotea katika maana ya maneno, akayatumia juu ya ni kitu gani maneno na badala yake akaacha yale yanayotambulika katika maana ya maneno katika lugha ya kiarabu?

[1] 16:40

[2] 09:06

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 166
  • Imechapishwa: 14/01/2017