al-Jaabiriy kuhusu ´Abdullaah al-Bukhaariy, Yahyaa al-Hajuuriy na ´Aliy al-Halabiy

Swali: Katika wasifu wa ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahiym al-Bukhaariy tumesoma ya kwamba wewe ni katika waalimu zake. Ni nini unachojua kuhusu Shaykh huyu mtukufu na manzilah yake ya kielimu? Tunasikia watu wanamponda na kusema kuwa ni katika wanafunzi wachanga.
Jibu: Jambo la kwanza amesema kweli aliyesema kuwa ni mwanafunzi wangu na kwamba mimi ni mwalimu wake.

Ndugu, Shaykh na Dr. ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahiym al-Bukhaariy ana elimu nyingi na uhafamu. Ana haki wakati aliporaddi makala mbovu na misingi mibovu ambayo ni ya Ibraahiym bin ´Aamir ar-Ruhayliy na wengineo ambao wanajitangaza na kujinasibisha na Salafiyyah.

Namjua tokea miaka 15 ya nyuma au kitu kama hicho. Uhakika ni kwamba tuna mawasiliano naye zaidi ya miaka 20 nyuma. Yalianza wakati wa vita vya pili vya khaliji bado tuko naye mawasiliano. Akija katika mji wenu ni lazima mstafidi kwake. Ninasema hivo kwa kuwa najua ni elimu pana ilioje alonayo na ufahamu.

Anayemponda ima ni katika wafuasi wa mpotevu, mtu wa Bid´ah na mjinga Yahyaa al-Hajuuriy, wafuasi wa mpotevu mwingine ´Aliy al-Halabiy anafanya kanuni na istilahi za wanachuoni kuwa siasa au wafuasi wa Dr. Ibraahiym ar-Ruhayliy – Allaah Atusamehe sisi na yeye.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=134483
  • Imechapishwa: 18/01/2017