Najua kuwa Hizb-ut-Tahriyr wanakemea hukumu bungeni. Kadhalika al-Ikhwaan al-Muslimuun. Ni kwa nini basi baadhi ya Hizb-ut-Tahriyr wameingia bungeni? Ni kwa nini al-Ikhwaan al-Muslimuun wameingia bungeni? Ni kwa nini al-Ikhwaan ni wenye kutofautiana baadhi wanasapoti bunge na wengine wanakemea? Mnayajua haya au hamyajui? Nini maana ya kipote hichi ikiwa wao wenyewe kwa wenyewe ni wenye kutofautiana. Hili tunalijua tangu tulipokuwa Syria kabla ya kuhamia hapa.

Punde tu nimeulizwa kuhusu vitabu ninavyonasihi vya Fiqh. Miongoni mwa vitabu nilivyotaja ni pamoja na “Fiqh-ul-Sunnah”. Nimetungwa na Sayyid Saabiq ambaye ni mmoja katika wakuu wa al-Ikhwaan al-Muslimuun Misri. Alikuwa ni katika watu wa karibu wa Hasan al-Bannaa (Rahimahu Allaah).

al-Ikhwaan al-Muslimuun wametofautiana juu ya kitabu na mtunzi huyu. Kuna kundi kwetu Dameski wanakisoma katika duara zao za kielimu. Mimi ndiye niliwanasihi kufanya hivo. Ukienda kwa al-Ikhwaan al-Muslimuun kaskazini mwa Syria Halab, wanasema kuwa kitabu hiki haifai kukifunza kwa sababu mtunzi ni Wahhaabiy. Lakini makundi yote mawili ni al-Ikhwaan al-Muslimuun.

Hawana mfumo wa kifikira. Hizb-ut-Tahriyr wanatofautiana na watu hawa wao wako na mfumo wa kifikira katika masuala kadhaa na si katika Uislamu kwa ueneaji wake.

al-Ikhwaan al-Muslimuun wako kwa miaka sitini sabini. Mpaka sasa hawajazalisha mwanachuoni hata mmoja ambaye wanaweza kurejea kwake ili kufasiriwa Aayah, kutambua Hadiyth Swahiy na dhaifu au kujua tofauti za wanachuoni. Hawajakuwa na mwanachuoni hata mmoja. Kwa hiyo yako wapi manufaa ya ulinganizi wao?

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (541)
  • Imechapishwa: 10/07/2020