Swali: Mwishoni nilipokuwa Kuwait, na kadhalika kwa baadhi ya ndugu Saudi Arabia, niliwasikia wakisema mara nyingi kwamba fulani atakuwa ni Khaliyfah wako. Dalili yao ni baadhi ya kanda zako au matukio ambapo uliwasifia baadhi ya ndugu. Unasemaje kuwaambia ndugu hawa?
Jibu: Ninatarajia kwamba watachukua nafasi yangu watu ambao ni bora kuliko mimi. Hata hivyo sijataja mtu yeyote na wala siwezi kufanya hivo. Kuna malengo gani ya yote haya?
Muulizaji: Wanachotaka ni macho kumkodolea mtu maalum.
al-Albaaniy: Allaah ndiye anajua zaidi hilo. Walidai kwamba nilisema hivo juu ya ndugu yetu [Abu Ishaaq] al-Huwayniy. Lakini sijasema hivo na sintolisema.
Muulizaji: Wanasema kuwa ulimtaja Shaykh Muqbil.
al-Albaaniy: Ndio, nilimsifia. Lakini sikusema kuwa atakuwa ni Khaliyfah wangu.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (320)
- Imechapishwa: 18/12/2014
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)