Swali: Je, una nasaha yoyote kwa ndugu wa Sunnah walioko Tunisia na ni ipi njia bora ya kuwa na uthabiti katika mfumo wa haki wa Salaf-us-Swaalih? Tunataraji utatuelekeza.

Jibu: Tunawausia ndugu zetu Tunisia na kwenginepo:

1- Wamche Allaah (Subhaanah).

2- Wamtakasie nia.

3- Wajifunze elimu yenye manufaa. Wajifunze na kutilia umuhimu kujifunza elimu yenye manufaa kutoka katika vyanzo vyake na watu wake. Wapupie hilo hata kama litahitajia kufanya Hijrah, kutoka sehemu kwenda nyingine na kusafiri kwa ajili ya kutafuta elimu kwa kiasi na itavyowezekana.

4- Walinganie katika dini ya Allaah kwa hekima, maneno mazuri na kuzungumza kwa njia bora zaidi.

5- Tunawatahadharisha mizozo, kutofautiana, kuhamana na kukatana wao kwa wao. Badala yake wanatakiwa wawe na umoja na walete suluhu na wapendane kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) kwa sababu wao ni ndugu. Waumini wote ni ndugu. Mmoja akikosea kutafutwe suluhu ya kulirekebisha pasi na uadui, maneno ya kujeruhi na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2136
  • Imechapishwa: 12/07/2020