Swali: Ni ipi hukumu ya Sujuud inayopigwa na wachezaji katika michezo yao wanapofikiwa na kile wanachokitaka? Imenukuliwa kutoka kwako kwamba unaonelea hilo limewekwa katika Shari´ah kisha baadaye ikanukuliwa kuwa umelikataza?

Jibu: Mtu wa kwanza aliyenukuu ni muongo na mimi sijasema kuwa hilo ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Hiyo sio neema. Mchezo wa mpira sio neema. Sujuud-ush-Shukr inakuwa wakati wa kupata neema mpya. Sujuud mahala kama hapa ni Bid´ah.

Kumepatikana nini kwa kucheza mpira? Waislamu wamefaidika nini na kucheza mpira? Isipokuwa tu kuwapoteza vijana wao. Hawajafaidika nao. Bali ni madhara kwa Waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-5-23.mp3
  • Imechapishwa: 09/11/2014