Swali: Ni ipi hukumu ya kula, kunywa au kufanya jimaa kwa kusahau katika swawm iliyopendekezwa?
Jibu: Mwenye kusahau swawm yake haiharibiki, ni mamoja ikiwa ni swawm iliypendekezwa au ya faradhi. Mwenye kusahau hachukuliwi wala swawm yake haivunjiki. Haya yanahusiana na kula na kunywa. Kwa kuwa haya ndio yaliyothibiti.
Lakini kuhusu kufanya jimaa haikuthibiti kwamba inaweza kuwa kwa kusahau. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuja yule mtu ambaye alimwambia kuwa amemwingilia mke wake ilihali amefunga, hakumwambia “Vipi, ulikuwa umesahau?” Hapana. Alimtolea fatwa ya kutoa kafara.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-14.mp3
- Imechapishwa: 14/11/2014
Swali: Ni ipi hukumu ya kula, kunywa au kufanya jimaa kwa kusahau katika swawm iliyopendekezwa?
Jibu: Mwenye kusahau swawm yake haiharibiki, ni mamoja ikiwa ni swawm iliypendekezwa au ya faradhi. Mwenye kusahau hachukuliwi wala swawm yake haivunjiki. Haya yanahusiana na kula na kunywa. Kwa kuwa haya ndio yaliyothibiti.
Lakini kuhusu kufanya jimaa haikuthibiti kwamba inaweza kuwa kwa kusahau. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuja yule mtu ambaye alimwambia kuwa amemwingilia mke wake ilihali amefunga, hakumwambia “Vipi, ulikuwa umesahau?” Hapana. Alimtolea fatwa ya kutoa kafara.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-14.mp3
Imechapishwa: 14/11/2014
https://firqatunnajia.com/al-fawzaan-kuhusu-mfungaji-kufanya-jimaa-kwa-kusahau/