Swali: Baadhi ya watu wanaeneza ujumbe huu na ni upi usahihi wake:

حَسْبُنَا اللَّـهُ سَيُؤْتِينَا اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَرَسُولُهُ إِنَّا إِلَى اللَّـهِ رَاغِبُونَ

“Anatutosheleza Allaah, karibuni Allaah atatupa katika fadhilah Zake na Mtume Wake; hakika sisi kwa Allaah ni wenye shauku.” (09:59)

Wanasema kuwa Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) ameapa na kusema ya kwamba hakuomba kwa du´aa hii baada ya Tashahhud ya mwisho kwa jambo zito isipokuwa Allaah alilifanya kuwa jepesi. Wasemaje juu ya hilo na ulimsikia akisema hivo?

Jibu: Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hatukumsikia na wala hatukusoma kwenye vitabu vyake. Ikiwa aliyenukuu haya ameyapata kwenye vitabu vyake Shaykh, basi atubainishie kwa kutwambia ni kitabu na kurasa fulani. Ama kumnasibishia Shaykh kitu kisichokuwa na uthibitisho, hili halijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (80) ttp://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_08_03_1433.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020