al-Fawzaan kuhusu kumpa kiungo mgonjwa anayehitajia

Swali: Je, inajuzu kupeana viungo kumpa mtu ambaye ni mgonjwa anayehitajia na ikiwa hakupewa anaweza kufa kwa sababu ya hilo?

Jibu: Ndio. Inajuzu kupeana viungo kwa sharti mbili:

1- Sharti ya kwanza: Yule anayetoa kiungo iwe hatoathirika kwa kufanya hivo. Kule kuchukua kutoka kwake hakutomuathiri.

2- Sharit ya pili: Yule anayepewa [kiungo hichi] awe atanufaika kwacho.

Katika hali hiyo itajuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majid%20%207%20-%205%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 06/10/2020