Kwa muheshimiwa Shaykh na ndugu mtukufu Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy – Allaah amuhifadhi na ampe mafanikio.

Aamiyn.

as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh

Amaa ba´d:

Nimesoma kitabu chako chenye thamani “al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal” na kuona kuwa ni chenye thamani na faida. Ni kitabu muhimu sana kwa leo ambapo kuna makundi na mapote mengi ambayo kwa masikitiko makubwa yanajinasibisha na Da´wah ya Uislamu. Hata hivyo ni jambo lenye kujulikana ya kwamba katika Uislamu kuna kundi na mfumo mmoja tu.

Kundi lenyewe ni la Ahl-us-Sunnah na mfumo ni wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Namna hiyo ndivyo alivowasifu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipotaja makundi na mapote yenye kwenda kinyume:

“Ni wale wenye kufuata yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

Sisi hatuna isipokuwa kundi limoja ambalo ni kundi la Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, mfumo mmoja ambao ni mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Imaam mmoja ambaye ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hatuyatambui makundi mengine yote, mifumo na kiongozi.

Kitabu chenu – Allaah akuhifadhi – ni chenye kutosheleza kwa kubainisha haki na kuraddi batili katika maudhui haya14. Allaah akujaze kheri kwa kazi nzuri ulioifanya ya kuweka haki wazi na kuraddi batili.

Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, ahli zake na Maswahabah zake.

Ndugu yenu katika Uislamu: Swaalih bin Fawzaan bin ´Abdillaah al-Fawzaan 1414/11/2715

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 05/07/2020