Swali: Kununua misahafu na kuiweka kwenye msikiti wa Makkah kwa nia ya swadaqah yenye kuendelea ni kitendo kinachojuzu?

Jibu: Ni tendo jema hili. Misahafu ilikuwa inanunuliwa wakati wa Salaf. Walikuwa wakiiuza. Huwezi kupata msahafu isipokuwa kwa njia ya kuununua. Vipi utaweza kupata msahafu ikiwa sio kwa njia ya kuununua? Je, wewe una uwezo wa kujiandikia msahafu wako mwenyewe? Nunua msahafu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14763
  • Imechapishwa: 21/06/2020