Swali: Ikiwa nimekaa katika kikao ambapo akaja mtu, wakaondoka waliokuwapo wakasimama kwa ajili yake, lakini mimi sikusimama – Je, ninawajibika kusimama? Je, waliomsimamia mgeni wana dhambi?
Jibu: Kusimama kwa ajili ya anayekuja si wajibu. Kitendo hicho ni katika maadili mema. Yule anayesimama kwa ajili ya kumsalimia mtu, kama kupeana naye mkono, khaswa kiongozi wa kikao na watu muhimu, hii ni katika tabia njema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama kwa ajili ya Faatwimah, naye (Radhiya Allaahu ´anhaa) akasimama kwa ajili yake. Vilevile Maswahabah walisimama kwa amri yake kwa ajili ya Sa´d bin Mu´aadh alipokuja kuhukumu Banuu Quraydhwah. Aidha Twalhah bin ´Ubaydullaah alisimama mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuja Ka´b ambaye Allaah alikuwa amekubali tawbah yake ambapo akasimama, akamsalimia, akampongeza, kisha akakaa. Haya ni katika mambo ya tabia njema. Aliyesimama afanye hivyo, na asiyesimama akakaa hakuna neno. Jambo hili ni lenye wasaa.
Kinachokazwa ni kusimama tu bila kitu. Kusimama kwa ajili ya utukufu tu. Ama kusimama ili kumlaki mgeni, kumkaribisha au kumsalimia na kumheshimu, hili ni jambo linalokubalika. Lakini kusimama watu wote huku yeye anakaa kwa ajili ya kumtukuza tu, bila sababu ya ulinzi wala huduma, hili halifai.
Kusimama kwa ajili ya mtu kuna aina tatu:
1 – Kusimama juu yake naye amekaa kwa ajili ya utukufu, kama wanavyofanya watu wa mataifa kwa wafalme wao na wakuu wao. Hili halijuzu. Ndiyo maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamuru watu wakae wakati alipowaswalisha hali ya kukaa na wao wakiwa wamesimama. Alipoona (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamesimama akasema:
”Karibu muanze kunitukuza kama wanavyowatukuza viongozi wao watu wa kigeni.”
2 – Kusimama kwa ajili ya mtu anapoingia au kutoka bila chochote, bila kumlaki na bila kumsaidia, bali kwa kutukuza tu. Dogo liwezalo kusemwa juu ya hili ni kwamba inachukiza. Maswahabah hawakuwa wanasimama kwa ajili ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapoingia walipo kutokana na walivyotambua kuwa anachukizwa na jambo hilo.
3 – Kusimama kwa ajili ya kumlaki mtu anayekuja, kama kumsalimia, kupeana naye mkono, kumkaribisha, kumkalisha mahali au mfano wa hivyo. Hili halina neno. Ni katika Sunnah kwa watu muhimu na wale wanaohitaji kukaribishwa. Kama walivyosimama Maswahabah kwa amri ya Mtume kwa ajili ya Sa´d bin Mu´aadh kumkaribisha na kumheshimu alipokuja kuhukumu Banuu Quraydhwah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
”Simameni kwa ajili ya bwana wenu.”
Wakamsimamia, wakamsalimia na wakamshusha.
Faatwimah alikuwa akisimama kwa ajili ya baba yake anapokuja, naye akisimama kwa ajili yake anapokuja. Aidha Twalhah bin ´Ubaydullaah at-Taymiy alisimama kwa ajili ya Ka´b kumsalimia na kumpongeza alipokuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) msikitini, akamsalimia, kupeana naye mkono, kisha akakaa. Haya yako katika aina hii ya tatu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/987/حكم-قيام-الرجل-لغيره
- Imechapishwa: 01/01/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/987/حكم-قيام-الرجل-لغيره
Imechapishwa: 01/01/2026
https://firqatunnajia.com/aina-tatu-ya-kusimama-kwa-ajili-ya-mtu-mwingine/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket