Swali: Je, kuchupa mipaka kwa waja wema kunapelekea katika shirki?
Jibu: Kuna aina mbili ya kuchupa mipaka:
1 – Kuchupa mipaka kwa namna ya kwamba mtu akawaomba pamoja na Allaah. Akawatukua kwa kuwashirikisha, kuwataka msaada na kuwawekea nadhiri. Hii ni shirki kubwa.
2 – Kuchupa mipaka kwao ambako sio shirki kubwa. Kwa mfano akawapapasa kwa kuona kwamba kitendo hicho kinamkurubisha mbele ya Allaah, anawasimamia wanapoingia au anasimama karibu na vichwa vyao kwa kuona kuwa kufanya hivo kunamkurubisha mbele ya Allaah. Hiyo ni miongoni mwa njia zinazopelekea katika shirki.
Swali: Vipi kuhusu kubusu viatu vya waja wema na akajipangusa navyo?
Jibu: Kitendo hichi kinaweza kumpelekea katika shirki kubwa. Lakini akiona kuwa matendo hayo – kuwabusu, kusimama kwa ajili yao na kadhalika – yananamkurubisha mbele ya Allaah, yanahitajia upambanuzi. Busu la kawaida na kupeana nao mkono hapana vibaya. Lakini kutafuta baraka kwa kugusa mikono, kofia zao na kadhalika, ni katika njia za shirki. Baadhi ya Suufiyyah na wengineo wanaweza kutumbukia katika mambo hayo. Mambo hayo yanafanywa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); yeye ndiye ambaye baraka inatafutwa kutoka kwake kwa jasho lake, mkono wake na nywele zake. Mambo haya ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na haifai kutumia kipimo kwake juu ya wengine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24508/حكم-الغلو-في-الصالحين-وما-يكون-شركا-منه
- Imechapishwa: 28/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket