Aina mbalimbali za kufanya upasuaji na hukumu zake

Kuhusu kujitibu kwa ajili ya kujifanya na kufuta uzuri, jambo hili limegawanyika aina mbili:

Aina ya kwanza: Ni mtu akaondoa kasoro alonayo.

Aina ya pili: Mtu anatafuta uzuri wa ziada.

Aina ya kwanza ambayo ni kuondosha kasoro inajuzu. Kwa mfano mtu pua yake imepinda basi inafaa kwake akafanya upasuaji ili kuondosha kasoro hii. Pua aina hii sio maumbile yake. Limepinda na anataka kuliweka sawa. Mfano mwingine mtu mwenye makengeza. Makengeza ni kasoro pasi na shaka yoyote. Iwapo mtu atataka kufanya operesheni kwa ajili ya kuondosha kasoro hii itafaa na hakuna kizuizi. Kwa sababu inahusiana na kuondosha kasoro.

Kwa mfano mtu pua yake ikakatwa kwa sababu fulani inafaa kwake kuweka pua nyingine badala yake? Inafaa. Kwa sababu huku ni kuondosha kasoro. Tukio hili lilitokea wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna pua ya mmoja katika Maswahabah ambayo ilikatwa katika vita ambapo mtu yule akatengeneza pua ya fedha. Lakini fedha ile ikawa inaoza na kutoa harufu mbaya. Fedha huoza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamruhusu kutengeneza pua ya dhahabu ambapo mtu yule akawa amefanya hivo. Je, huku ni kutafuta urembo na uzuri au ni kuondosha kasoro? Ni kuondosha kasoro.

Aina ya pili ambayo ni kutafuta urembo na uzuri wa ziada ni jambo ambalo halijuzu. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wale wenye kutengeneza mwanya kwa ajili ya kutafuta uzuri. Pia amemlaani yule mwenye kuunganisha nywele juu ya nywele zake na mfano wa hayo.

Inajuzu kufanya upasuaji kwa ajili ya kufanya maziwa ima yakawa makubwa au yakawa madogo? Huku ni kutafuta urembo na uzuri wa ziada. Isipokuwa ikiwa kama mwanamke huyu mwenye matiti madogo ambaye mtoto wake hapati maziwa na hivyo anataka kufanya matibabu kwa ajili ya hilo. Huyu pengine tukasema kuwa hakuna ubaya kufanya hivo. Ama kufanya upasuaji kwa ajili ya kutafuta uzuri na urembo haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (50) http://binothaimeen.net/content/1144
  • Imechapishwa: 19/06/2019