Swali: Haafidhw Ibn Kathiyr ametaja katika ”al-Bidaayah wan-Nihaayah” kuhusu wasifu wa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) kwamba al-Bayhaqiy amepokea kutoka kwa Imaam Ahmad kuwa amesema kuhusiana na maneno Yake Allaah (Ta´ala):
وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا
”… na atakapokuja Mola Wako na Malaika safu kwa safu.”[1]
kwamba maana yake ni amekuja amri Yake.”
al-Khallaal ameeleza kutoka kwa Imaam Ahmad kwamba amesema kuhusu sifa za Allaah:
”Tunazipitishakama zilivyokuja bila namna na bila maana.”
Kunasemwa nini kuhusu mapokezi hayo?
Jibu: Riwaya hiyo ni makosa na haikusihi kutoka kwa Ahmad (Rahimahu Allaah). Kwa sababu msingi ni kutopindisha maana ya maandiko ya sifa za Allaah, bali tunazipitisha kama zilivyokuja. Maneno Yake Allaah:
وَجَاءَ رَبُّكَ
”… na atakapokuja Mola Wako… “
Asili yake ni kuja Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala) siku ya Qiyaamah, kama Alivyosema (Jalla wa ´Alaa):
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ
“Je, wanangojea nini isipokuwa Malaika wawajie au awafikie Mola?”[2]
Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) atakuja siku ya Qiyaamah kwa ajili ya kuhukumu baina ya waja Wake. Inahusiana na ujio unaolingana na utukufu Wake. Haijuzu kutafsiri kwa kupindisha maana.
Wapo baadhi ya wafasiri wa Qur-aan waliotaja maneno haya kwamba maana yake ni kuwa amri ya Mola wako ikaja, jambo ambalo ni makosa. Hata kama ingesihi kutoka kwa Ahmad, basi ni kosa alilofanya. Kwa sababu maandiko mengine yanathibitisha kinyume chake. Kwa kuwa kanuni ya Ahmad na Salaf, ambao ni Maswahabah na wanafunzi wao, ni kutopindisha maana. Bali wanayapitisha maandiko juu ya dhahiri yake bila kuyafanyia namna, kulinganisha wala kuyapotosha majina na sifa za Allaah. Huu ndio msingi wa Salaf. Kwa hivyo ikija riwaya isiyo ya kawaida kutoka kwa Ahmad, basi aidha ni batili au ni makosa aliyoteleza. Si yeye wala mwengine yeyote hakuna ambaye amekingwa na kukosea.
[1] 89:22
[2] 6:158
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30994/ما-معنى-المجيء-في-قوله-تعالى-وجاء-ربك
- Imechapishwa: 24/09/2025
Swali: Haafidhw Ibn Kathiyr ametaja katika ”al-Bidaayah wan-Nihaayah” kuhusu wasifu wa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) kwamba al-Bayhaqiy amepokea kutoka kwa Imaam Ahmad kuwa amesema kuhusiana na maneno Yake Allaah (Ta´ala):
وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا
”… na atakapokuja Mola Wako na Malaika safu kwa safu.”[1]
kwamba maana yake ni amekuja amri Yake.”
al-Khallaal ameeleza kutoka kwa Imaam Ahmad kwamba amesema kuhusu sifa za Allaah:
”Tunazipitishakama zilivyokuja bila namna na bila maana.”
Kunasemwa nini kuhusu mapokezi hayo?
Jibu: Riwaya hiyo ni makosa na haikusihi kutoka kwa Ahmad (Rahimahu Allaah). Kwa sababu msingi ni kutopindisha maana ya maandiko ya sifa za Allaah, bali tunazipitisha kama zilivyokuja. Maneno Yake Allaah:
وَجَاءَ رَبُّكَ
”… na atakapokuja Mola Wako… ”
Asili yake ni kuja Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala) siku ya Qiyaamah, kama Alivyosema (Jalla wa ´Alaa):
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ
“Je, wanangojea nini isipokuwa Malaika wawajie au awafikie Mola?”[2]
Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) atakuja siku ya Qiyaamah kwa ajili ya kuhukumu baina ya waja Wake. Inahusiana na ujio unaolingana na utukufu Wake. Haijuzu kutafsiri kwa kupindisha maana.
Wapo baadhi ya wafasiri wa Qur-aan waliotaja maneno haya kwamba maana yake ni kuwa amri ya Mola wako ikaja, jambo ambalo ni makosa. Hata kama ingesihi kutoka kwa Ahmad, basi ni kosa alilofanya. Kwa sababu maandiko mengine yanathibitisha kinyume chake. Kwa kuwa kanuni ya Ahmad na Salaf, ambao ni Maswahabah na wanafunzi wao, ni kutopindisha maana. Bali wanayapitisha maandiko juu ya dhahiri yake bila kuyafanyia namna, kulinganisha wala kuyapotosha majina na sifa za Allaah. Huu ndio msingi wa Salaf. Kwa hivyo ikija riwaya isiyo ya kawaida kutoka kwa Ahmad, basi aidha ni batili au ni makosa aliyoteleza. Si yeye wala mwengine yeyote hakuna ambaye amekingwa na kukosea.
[1] 89:22
[2] 6:158
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30994/ما-معنى-المجيء-في-قوله-تعالى-وجاء-ربك
Imechapishwa: 24/09/2025
https://firqatunnajia.com/aidha-haikuthibiti-kwa-ahmad-au-alikosea/