Swali 292: Je, inafaa sasa kusema kuhusu mtu aliyesifiwa kwa kheri:

“Imemthubutikia.”?

Jibu: Kwa mujibu wa ilivyokuja katika Hadiyth, ndiyo. Kwa sababu hiyo Abu Thawr alikuwa akisema:

“Hakika Ahmad bin Hanbal yuko Peponi.”

Kwa sababu amesifiwa kwa kheri. Ingawa maoni maarufu kwa Ahl-us-Sunnah ni kwamba hakuthibitishwi Pepo isipokuwa kwa yule aliyethibitishiwa kwa dalili, lakini maoni haya ni yenye nguvu na yamefahamishwa na dalili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 107
  • Imechapishwa: 22/05/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´