Umeandika kwenye barua yako:
“Walichunguza khabari yake na kumpa udhuru kwa makosa aliyotumbukiaemo.”
1- Ni makosa yepi anayotakiwa kupewa udhuru? Si ni makosa madogomadogo yanayotokana na Ijtihaad? Je, makosa ya al-Bannaa ni madogo ili aweze kupewa udhuru? Je, al-Bannaa alikuwa ni Mujtahid mwenye haki juu ya hilo? Ni wanachuoni wepi alisoma elimu ya Kishari´ah kwao?
2- Wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wamekubaliana juu ya kwamba hakuna kupewa udhuru katika makosa ya ki-´Aqiydah. Vitabu visivyoweza kudhibitiwa ambavyo ambavyo vimewaraddi watu wa Bid´ah, kuanzia wakati wa Taabi´uun mpaka hii leo, vinatoa ushahidi juu ya hilo.
3- Mashaykh uliyowataja ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Lau wangelijua kuwa al-Bannaa alikosea katika mambo ya kimsingi na ´Aqiydah, basi wasingelimpa udhuru.
4- Kusema ya kwamba walimpa udhuru si jengine isipokuwa ni madai yako tu. Kama una linalothibitisha hilo, basi onyesha. Hili unaweza kulikwepa kwa [kuleta] wale ambao wameshafariki. Ama Shaykh ´Abdul-´Aziyz, yupo na unajulikana msimamo wake juu ya watu hawa. Yeye ndio kiongozi na kiigizo chetu. Tunajua kuwa anaraddi kila kosa analosikia na kulijua pasi na kujali linatoka kwa nani. Anaraddi hata kwa kosa katika mambo madogomadogo. Ameraddi makosa yasiyodhitibika. Ninaweza kumwandikia na kumuuliza kama ni kweli kwamba fulani anadai kuwa unampa udhuru Hasan al-Bannaa katika makosa ya ki-´Aqiydah.
5- Lau tutachukulia kuwa ni kweli kuna mwanachuoni anayempa udhuru kwenye makosa yake ya ki-´Aqiydah, basi udhuru wake unazingatiwa kuwa ni wenye kwenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
6- Anayempa udhuru anasema kuwa mtu asimraddi? Ikiwa anasema hivo, basi amewasaidia watu wa Bid´ah wenye kueneza ufisadi katika ardhi.
- Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Radd-ul-Jawaab, uk. 22-23
- Imechapishwa: 05/07/2020

Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Radd-ul-Jawaab, uk. 22-23
Imechapishwa: 05/07/2020
https://firqatunnajia.com/ahmad-an-najmiy-anamjibu-ibn-jibriyn-5/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)