Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
عن أَبي رُقَيَّةَ تَمِيم بن أوس الداريِّ رضي الله عنه: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (الدِّينُ النَّصِيحةُ) قلنا: لِمَنْ؟ قَالَ: (لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلأئِمَّةِ المُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ))
181- Abu Ruqayyah Tamiym bin Aws ad-Daariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Dini ni kupeana nasaha.” Tukasema: “Kwa nani?” Akasema: “Kwa Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na waislamu wa kawaida.”[1]
Miongoni mwa nasaha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kutetea Shari´ah yake na kuihami. Kuitetea ili asiivamie yeyote. Kuitetea ili asizidishe yeyote kisichomo. Pambana na Ahl-ul-Bid´ah kwa njia ya kimaneno na kimatendo na kiimani. Bid´ah mlango wake ni mmoja: kila Bid´ah ni upotevu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kila Bid´ah ni upotevu.”
Hakuvuliwi katika hili si Bid´ah ya kimaneno, kimatendo wala kiimani. Kila kinachoenda kinyume na uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale aliyokuja nayo, sawa ikiwa ni katika ´Aqiydah, maneno na matendo, ni Bid´ah. Kwa hiyo miongoni mwa nasaha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wewe kuwapiga vita Ahl-ul-Bid´ah kama jinsi wao wanavoipiga vita Sunnah. Wakiipiga vita kwa maneno na wao watapigwa vita kimaneno. Wakiipiga vita kimatendo na wao watapigwa vita kimatendo. Mtu anavuna kile alichopanda. Kufanya hivo ni katika nasaha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Muslim.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/390-391)
- Imechapishwa: 27/07/2025
Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
عن أَبي رُقَيَّةَ تَمِيم بن أوس الداريِّ رضي الله عنه: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (الدِّينُ النَّصِيحةُ) قلنا: لِمَنْ؟ قَالَ: (لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلأئِمَّةِ المُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ))
181- Abu Ruqayyah Tamiym bin Aws ad-Daariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Dini ni kupeana nasaha.” Tukasema: “Kwa nani?” Akasema: “Kwa Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na waislamu wa kawaida.”[1]
Miongoni mwa nasaha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kutetea Shari´ah yake na kuihami. Kuitetea ili asiivamie yeyote. Kuitetea ili asizidishe yeyote kisichomo. Pambana na Ahl-ul-Bid´ah kwa njia ya kimaneno na kimatendo na kiimani. Bid´ah mlango wake ni mmoja: kila Bid´ah ni upotevu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kila Bid´ah ni upotevu.”
Hakuvuliwi katika hili si Bid´ah ya kimaneno, kimatendo wala kiimani. Kila kinachoenda kinyume na uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale aliyokuja nayo, sawa ikiwa ni katika ´Aqiydah, maneno na matendo, ni Bid´ah. Kwa hiyo miongoni mwa nasaha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wewe kuwapiga vita Ahl-ul-Bid´ah kama jinsi wao wanavoipiga vita Sunnah. Wakiipiga vita kwa maneno na wao watapigwa vita kimaneno. Wakiipiga vita kimatendo na wao watapigwa vita kimatendo. Mtu anavuna kile alichopanda. Kufanya hivo ni katika nasaha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Muslim.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/390-391)
Imechapishwa: 27/07/2025
https://firqatunnajia.com/ahl-ul-bidah-ni-lazima-wapigwe-vita/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket