Afanye nini asiyepata swadaqah ya kutoa?

Swali: Mtu afanye nini ikiwa hana mali ya kutoa; si pesa wala kitu kingine?

Jibu: Atamke kheri. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa Mola Wake atamsemeza. Kutakuwa hakuna baina yake na Yake mwenye kutarjumu. Atatazama kuliani mwake na asione isipokuwa yale aliyoyatanguliza. Atatazama kushotoni mwake na asione isipokuwa yale aliyoyatanguliza. Atatazama mbele yake na asione isipokuwa yale aliyoyatanguliza. Hivyo basi, uogopeni Moto ijapo kwa kipande cha tende. Asiyepata kipande cha tende basi aseme neno zuri.”[1]

Asiyepata basi atamke neno zuri, kama kusema ”Allaah akusaidie”, ”Allaah akusahilishie jambo lako” na mfano wake.

[1] al-Bukhaariy (3595) na Muslim (1016).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2449ماذا-يفعل-من-لا-يجد-مالا-او-شيىا-ينفقه
  • Imechapishwa: 24/10/2024