Aendelee kupangusa juu ya soksi alizozivaa alipofanya Tayammum?

Swali: Maji yakikosekana kisha akafanya Tayammum na akavaa soksi, kisha baadaye maji yakapatikana. Je, atapangusa juu yake?

Jibu: Atazivua, kwa sababu mwanzoni alifuta juu yake bila ya twahara ya maji. Twahara ya udongo ni pungufu ukilinganisha na twahara ya maji. Kwa hivyo asipanguse juu yake isipokuwa baada ya twahara kamili aliyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24743/هل-يمسح-على-الجوربين-من-لبسهما-بعد-تيمم
  • Imechapishwa: 05/12/2024