Swali: Je, mchawi anaadhibiwa au anauliwa?

Jibu: Kinachotambulika kutoka kwa Mtume (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) ni kwamba alimwacha na hakumuua. Pengine alifanya hivo kwa ajili ya (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) kuwalainisha na kuwalingania kwa Allaah. Jengine ni kwa sababu alikuwa myahudi anayetambulika. Lakini akifanya muislamu anauliwa, kwa sababu uchawi ni kuritadi kutoka katika Uislamu. Mtu hawezi kufanya uchawi isipokuwa kwa msaada wa mashaytwaan. Mchawi anauliwa kama alivofanya ´Umar.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24069/ما-عقوبة-الساحر-المسلم-وغير-المسلم
  • Imechapishwa: 22/08/2024