Achague yupi katika wachumba hawa?

Swali: Dada huyu anasema amejiwa na wanamme mmoja anayenyoa ndevu, anayevaa Isbaal, msikilizaji muziki na anayetazama musalsal kwa mwanamke ambaye amehifadhi Kitabu cha Allaah na ni mwanafunzi. Je, aolewe nao au atafute wengine kwa kuwa anasema kuwa pengine baadaye wakaongoka?

Jibu: Hapana. Akitubu na kurejea kwa Allaah tawbah sahihi [olewa naye]. Ama kuolewa naye ilihali bado yuko katika hali hii kwa kutarajia pengine akaongoka katika siku za mbele, hapana:

“Atapokujieni yule ambaye mmemridhia dini na amaana yake, basi muozesheni.”

Check Also

Kaoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab ambaye hataki kuingia katika Uislamu

Swali: Nimeoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab kabla ya kuwa na msimamo, na nimepewa fatwa na baadhi …